Lugha ina vipashio vinne navyo ni kama vifuatavyvo:
1 Sauti
2 Mofimu/silabi
3 Neno
4 Sentensi
Mofimu ndicho kipashio kidogo sana cha lugha. Sauti huunda silabi. Silabi ni mpigo mmoja wa sauti unapotamka. k.m neno sentensi lina silabi tatu, nazo ni se-nte-nsi. Kama inavyoonekana, 'sentensi' ni neno ambalo limeundwa kwa silabi tatu.
Naam, sauti ikishaunda silabi, silabi ikaunda neno, neno nalo linaunda nini? Tuone mfano wa maneno yafuatayo hapa chini:
Sentensi hii haisomeki vizuri.
Sentensi hii hapa juu imeundwa kwa manano manne: sentensi + hii + haisomeki + vizuri. Hivyo basi tunapata kuwa neno au maneno yanaunda sentensi. Yaani sentensi ni neno au fungu la maneno yanayobeba ujumbe uliokamilika, na sentensi ndicho kipashio cha juu sana cha lugha