Friday, 18 April 2014

Uchambuzi wa Ushairi

Istilahi zitumikazo katika Ushairi
Mizani
Ni silabi ambazo zinapatikana katika kila neno.

Vina
Ni silabi zinazopatikana kila mwisho wa kipande cha ubeti. Katika mashairi ya tenzi, kina cha kila mshororo wa mwisho kinaitwa kina cha bahari.

Mshororo
Ni mstari katika kila ubeti.
*Mstari toshelezi ni mstari ulio na mizani inayolingana na mishororo mingine.
*Mshata ni mshororo usiojitosheleza kwa idadi ya mizani.
*Mwanzo ni mshororo wa kwanza katika kila ubeti.
*Mloto ni msororo wa pili katika kila ubeti.
*Mleo ni msororo wa tatu katika kila ubeti.
*Kituo/kiishio ni mshororo wa mwisho usiorudiwarudiwa katika kila ubeti. Kituo kinachorudiwarudiwa katika kila mshororo, kinajulikana kama, kiitikio, kibwagizo, kipokeo au mkarara.

Ukwapi
Ni kipande cha kwanza cha ubeti.

Utao
Ni kipande cha pili cha ubeti.

Mwandamizi
Ni kipande cha tatu cha ubeti

Ukingo
Ni kipande cha nne cha ubeti.

_____ukwapi____, __utao_____, ______mwandamizi_, ____ukingo___.

Ubeti
Ni fungu la mishororo ambayo aghalabu injitosheleza.

Urari
Ni utaratibu wa kupanga silabi zinazorudiwarudiwa katika kila mshororo wa ubeti.

Arudhi
Ni kanuni zinazoongoza utunzi wa ushairi. Arudhi huzingatia mpangilio wa vina, beti, mishororo, mizani, vipande, kituo (kama kimerudiwa katika kila ubeti au la).

 

 

No comments:

Post a Comment